Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Muhammad Twawiil amesema “Watumishi wetu wanasafisha uwanja wa katikati ya haram mbili na eneo linalozunguka Ataba tukufu kwa kutumia mitambo maalum ya kisasa”.
Akaongeza kuwa “Kazi ya usafi imeanza baada ya kukamilika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kwa lengo la kuweka mazingira mazuri kwa mazuwaru na kujiandaa na matukio mengine ya kitamaduni na kidini katika siku zijazo”.
Akabainisha kuwa “Kitengo kinafanya kazi kubwa ya kusafisha maeneo yote yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya, ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na kupokea mazuwaru wanaoendelea kuja kuzuru malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Kitengo kinacho simamia uwacha wa katikati ya haram mbili tukufu, kimetoa huduma tofauti kwa mamilioni ya watu waliokuja kufanya ziara ya Arubaini katika mji mtukufu wa Karbala.