Atabatu Abbasiyya imekamilisha majlisi za kuomboleza Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu, imehitimisha majlisi za kuomboleza Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) zilizokuwa zikifanywa ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Majlisi hizo ziliratibiwa na idara ya tablighi chini ya mradi wa Ummul-Banina (a.s).

Siku tatu zilihusisha mihadhara ya kidini, qawsida na tenzi za kuomboileza kutoka kwa Ali Basha Karbalai.

Majlisi zilikuwa na maudhui tofauti, miongoni mwa maudhui hizo ni, misingi ya adhari katika khutuba za Imamu Zainul-Aabidina na Bibi Zainabu (a.s).

Kulikuwa na baadhi ya mada za kijamii, kidini, kiaqida sambamba na kuangazia mapinduzi ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: