Kitengo cha malezi na elimu kinaendelea na ratiba ya kuwajengea uwezo watumishi wa shule za Al-Ameed.

Kitengo cha malezi na elimu katika Atabatu Abbasiyya kinaendelea na ratiba ya kuwajengea uwezo watumishi wa shule za Al-Ameed katika kujiandaa na mwaka mpya wa masomo.

Ratiba hiyo inalenga kuboresha uwezo wa walimu, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kitengo ili kuwafanya waendane na maendeleo ya dunia katika sekta ya ufundishaji wa kisasa.

Mkakati huu unatokana na mtazamo wa kitengo wa kuweka mazingira bora ya ufundishaji na usomaji.

Kitengo cha malezi na elimu kinafanya kila kiwezalo katika kuwajengea uwezo walimu na kuwafanya waendane na viwango vinavyohitajika katika shule zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: