Dua hiyo tukufu husomwa katika mazingira tulivu yaliyojaa Baraka za muhusika wa dua hiyo, kwa ushiriki wa mazuwaru wa haram tukufu.
Watumishi wa kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) huweka mazingira mazuri ya usomaji wa Dua-Nudba, kwa kuandaa vitabu vya dua, sehemu maalum ya kusomea dua, kupuliza marashi sambamba na kutoa huduma zingine zitakazohitajika.