Ugeni kutoka Uingereza umesifu utaratibu wa Atabatu Abbasiyya katika kutunza mali-kale.
Yamesemwa hayo wakati ugeni huo ulipotembelea Ataba tukufu na kuangalia kazi zinazofanywa na kituo cha kutunza turathi chini ya kitengo cha elimu na utamaduni.
Makamo rais wa kitengo cha habari Sayyid Jasaam Saidi amesema “Ugeni umehusisha wasomi wa kisekula na wanafunzi wa chuo kutoka nchini Uingereza, wametembelea Atabatu Abbasiyya na Markazi Alfadhli kuangalia utunzaji wa turathi”.
Akaongeza kuwa “Wageni wameangalia njia zinazotumika kutunza nakala-kale za kihistoria, wamepongeza utendaji wa kituo, wakaonyesha nia ya kuleta nakala-kale zao zije kufanyiwa matengeneza katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.