Idara ya wahadhiri katika Atabatu Abbasiyya tawi la wanawake, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Mtume (s.a.w.w).
Mhadhiri wa majlisi Shekhe Arkanu Tamimi amesema “Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imepambwa na muhadhara kuhusu historia ya Mutume Muhammad (s.a.w.w) na kazi kubwa aliyofanya ya kufundisha Dini tukufu ya Uislamu sambamba na kufafanua mabadiliko makubwa aliyofanya kwa mwanaadamu na Jamii”.
Akaongeza kuwa “Majlisi imeelezea historia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na athari yake katika uongozi, maadili, elimu, na jinsi alivyo mjenga mwanaadamu na kutengeneza jamii bora ya waislamu”.
Akabainisha kuwa “Majlisi imehudhuriwa na kundi kubwa la wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).