Majmaa ya Atabatu Abbasiyya imetaja huduma ilizotoa kwa mazuwaru wa Arubaini katika kituo cha Zurbatwiyya.

Atabatu Abbasiyya tukufu imetaja huduma zulizotolewa na Majmaa yake katika kituo cha Zurbatwiyya kilichopo mpakani kwa mazuwaru wa Arubaini, imesema kuwa wanufaika wa huduma zake wamefika mil 2.4.

Takwimu za Majmaa ya Atabatu Abbasiyya katika utoaji wa huduma kwa mazuwaru kwenye mji wa Zurbatwiyya wakati wa ziara ya Arubaini kuanzia mwezi 5 hadi 24 Safar mwaka 1446h imefika mazuwaru 2,482,700.

Takwimu zinaonyesha kuwa, Majmaa imegawa sahani za chakula 657,500, chupa za maji ya kunywa 1,667,150, matunda 34,400, juisi 4,000, vifurushi vya tende 48,000, mikate 71,650.

Majmaa ya Atabatu Abbasiyya inaendelea kuhudumia mazuwaru wanaofika kwenye kituo hicho wakielekea kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein kwa kuchelewa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: