Mhadhiri wa majlisi hiyo Shekhe Ali Abu Hawaatim Twaiy amesema “Majlisi inalenga kutambulisha utukufu wa Mtume, Qur’ani, Riwaya na dua zilizopokewa kutoka kwa Ahlulbait (a.s) zinazomtambulisha Mtume (s.a.w.w)”.
Akaongeza kuwa “Majlisi imehuduriwa na watumishi wa malalo tukufu na kundi kubwa la mazuwaru, itaendelea kwa muda wa siku tatu, tunaeleza historia ya Mtume (s.a.w.w) na kazi kubwa aliyofanya ya kutangaza Dini ya kiislamu”.
Akasema kuwa “Majlisi zitajikita katika kueleza mabadiliko aliyofanya (s.a.w.w) kwa mwanaadamu na jamii, majlisi hizi ni sehemu ya ratiba maalum ya Atabatu Abbasiyya katika kuomboleza kifo chake (s.a.w.w)”.