Idhaa ya Alkafeel inafanya shindano la Shafiul-Ummah kwa wanawake.

Idhaa ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya inafanya shindano la (Shafiul-Ummah) sambamba na maombolezo ya kifo cha Mtume (s.a.w.w).

Idhaa imebainisha kuwa mwisho wa kushiriki shindano hilo ni tarehe 29 ya mwezi huu wa Safar, sawa na tarehe 3/9/2024m, watachaguliwa washindi watatu kwa njia ya kura kutoka kwa wenye majibu sahihi.

Washindi wataenda kupokea zawadi zao katika idara ya Idhaa ya Alkafeel iliyopo kwenye jengo la Swidiqatu-Twahirah (a.s) ghorofa ya tato, mtaa wa Mulhaq jirani na chuo cha Swahibu Zamaan (a.f) mkabala na mtaa wa Usrah.

Kwa ushiriki bonyeza link ifuatayo: (https://forms.gle/1DYMojUdyJU1MrMf8).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: