Chuo kikuu cha Al-Ameed kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Mhadhiri alikuwa ni rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu Shekhe Swalahu Karbalai, ameongea kuhusu sifa nzuri za Mtume (s.a.w.w).
Akaeleza historia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na jihadi yake katika njia ya Mwenyezi Mungu, sambamba na kufafanua matatizo aliyopitia hadi roho yake ilipoenda kwa Mola wake mtukufu.