Maukibu ya chuo kikuu cha Alkafeel inahudumia mazuwaru wanaenda katika malalo ya Imamu Ali (a.s) kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Maukibu iliyopo katika barabara ya Imamu Ali (a.s) karibu na daraja ya Thauratu-Ishrina, inatoa huduma siku zote za ziara, miongoni mwa huduma hizo ni kugawa chakula na maji kwa mazuwaru.
Maukibu inahudumia mazuwaru na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awawezeshe kwenda kumtembelea Mtume Muhammad (s.a.w.w) hapa Duniani na wapate shifaa yake Akhera.
Maukibu ya chuo kikuu cha Alkafeel hutoa huduma kwa mazuwaru katika kila tukio la kidini, huwapa mahitaji yao na kuandaa sehemu ya kupumzika.