Muheshimiwa Sayyid Swafi amefuatana na rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, Muhandisi Dhiyaau Majidi na baadhi ya wasimamizi wa mradi kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya mwisho kabla ya kufunguliwa madi.
Sayyid Swafi amesikiliza maelezo kuhusu utengenezaji wa dawa bora zinazokidhi vigezo vya kimataifa, sambamba na mitambo ya kisasa iliyopo kwenye kiwanda hicho, mchango wake katika kutosheleza soko la ndani kupitia kazi zinazofanywa na raia wazalendo.
Sayyid Swafi amepongeza kazi nzuri iliyofanywa ya kukamilisha maandalizi yote katika mradi huo unaosaidia sekta ya utengenezaji wa dawa hapa Iraq.
Kiwanda hicho ni moja ya miradi mikubwa katika Atabatu Abbasiyya utakaochangia kupatikana kwa dawa zitakazonufaisha mamilioni ya watu.