Kupitia majlisi ya kuomboleza.. Atabatu Abbasiyya imeomboleza kifo cha Mtume (s.a.w.w)

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kimeomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) kupitia majlisi ya kuomboleza.

Mhadhiri wa majlisi Shekhe Muhammad Kuraitwi amesema “Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), imehudhuriwa na idadi kubwa ya watumishi wa Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa “Majlisi ilikuwa na mada nyingi, miongoni mwa mada hizo ni: Historia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), utukufu wake katika kulinda Dini ya kiislamu, changamoto alizopambana nazo wakati anatangaza Dini na athari ya kifo chake kwa waislamu”.

Akabainisha kuwa “Majlisi imejikita katika kueleza mabadiliko aliyofanya Mtume (s.a.w.w) kwa wanaadamu, akasema “Majlisi ni sehemu ya ratiba maalum ya kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika Ataba tukufu”.

Atabatu Abbasiyya tukufu huhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) kwa lengo la kulinda misingi ya uislamu na kujenga misingi bora ya kiroho na kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: