Mmoja wa washiriki wa maukibu hiyo kutoka Atabatu Husseiniyya Sayyid Haidari Abbasi Fadhwalah amesema “Maukibu imeanza matembezi yake ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikapita katikati ya haram mbili tukufu hadi kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s) kwenda kumpa pole kwa msiba huo”.
Akaongeza kuwa “Baada ya kuwasili katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s), ikafanya majlisi ya kuomboleza iliyopambwa na qaswida na tenzi zilizotaja dhulma aliyofanyiwa Mtume (s.a.w.w)”.
Akabainisha kuwa “Watumishi wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala, hufanya maukibu maalum ya kuomboleza kumbukumbu za vifo vya Ahlulbait (a.s)”.