Atabatu Abbasiyya tukufu imebadilisha bendera ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imetolewa bendera ya rangi nyeusi na kuwekwa nyekundu, kufuatia kuingia kwa mwezi wa Rabiul-Awwal (1446h).
Watumishi wa Ataba wameondoa mabango meusi kwenye minara, korido na sehemu zingine zote.
Makamo rais wa kitengo cha kusimamia haram tukufu Shekhe Zainul-Aabidina Quraish amesema “Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamekamilisha kazi ya kuondoa mapambo meusi katika haram tukufu ambayo huwekwa mwanzoni mwa mwezi wa Muharam hadi siku ya mwisho ya mwezi wa Safara, sambamba na kuingia mwezi wa Rabiul-Awwal na kuisha kwa mienzi ya huzuni katika familia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambapo mazingira ya huzuni hudumu kwa miezi miwili mfululizo na waombolezaji huja Karbala kutoka kila sehemu ya dunia”.
Akaongeza kuwa “Kazi ya kuondoa mapambo meusi ilitanguliwa na kazi ya kubadilisha bendera ya kubba tukufu, kutoa bendera nyeusi na kuweka nyekundu, sambamba na kuondoa mabango yote yanayoashiria huzuni yaliyokuwa yamewekwa kwenye minara, korido, milango na kwenye kuta za ndani na nje ya haram tukufu, ambayo yamedumu kwa miezi miwili mfululizo”.