Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wameaga miezi miwili ya huzuni Muharam na Safar, kwa kufanya kitendo cha kuhuisha utiifu katika haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kitendo hicho cha kiibada kimefanywa ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na kundi kubwa la watumishi wa Ataba tukufu.
Kitengo cha kiibada hufanywa Jumanne na Alkhamisi ya kila wiki, hufunguliwa kwa kusoma ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na watumishi wa malalo tukufu wakiwa wamesimama kwa mistari mbele ya kaburi takatifu, kisha hufuatia wimbo wa (Lahnul-Ibaa).