Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya semina kuhusu maelezo na ujumbe wa kiofisi kwa watumishi wake.
Mkufunzi wa semina ni Sayyid Hussein Hamidi Audah, amefundisha mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kutambua washiriki, mbinu za kuandaa ujumbe wa kiofisi, kufafanua viwango vya ofisi kwa mpangilio wa kiidara, sambamba na kufafanua aina za mahitaji maalum katika uandaaji wa ujumbe.
Semina hiyo ni sehemu ya kuwajengea uwezo watumishi katika kuandaa ujumbe na maelekezo maalum ya kiofisi.
Semina imefanyika ndani ya ukumbi wa Naafidhu-Albaswirah katika jengo la Imamu Swadiq (a.s) la vitengo vya Ataba kwa muda wa siku tatu.