Majmaa-Ilmi inawapa mitihani wanafunzi wa tahfiidh

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imewapa mitihani ya kuwapima wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani tukufu.

Kiongozi wa idara ya tahfiidh katika Maahadi ya Qur’ani tawi la Baghdad chini ya Majmaa Sayyid Ali Khalidi amesema “Majmaa imewapa mtihani wanafunzi wa mradi wa tahfiidh katika jengo la Alqami mkoani Karbala chini ya usimamizi wa walimu wa idara ya tahfiidh katika Maahadi”.

Akaongeza kuwa “Mitihani ya kupima uwezo wa kuhifadhi Qur’ani tukufu hufanywa kila mwezi, kwa lengo la kuangalia ukamilifu na upungufu wao ili kuwawezesha kuhifadhi haraka na kwa ubora kupitia kuimarisha uwezo wao wa kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Akafafanua kuwa “Maahadi inatilia umuhimu mkubwa mradi wa kuhifadhi Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baghdad, huwapa semina mbalimbali wanafunzi wa tahfiidh kutoka maeneo tofauti ya mkoa, kwa lengo la kutengeneza kizazi cha vijana waumini wanaoshikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu pamoja na kizazi kitakasifu (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: