Atabatu Abbasiyya tukufu imebadilisha pazia za milango ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kuondoa pazia nyeusi na kuweka pazia mpya za rangi ya kijani.
Haram tukufu ya Ataba imetandikwa mazulia mapya yenye ubora wa hali ya juu.
Mabadiliko hayo yanafanywa baada ya kuisha miezi ya huzuni Muharam na Safar, sehemu zingine za haram pia zimefanyiwa usafi mkubwa, kama vile mapambo, milango na madirisha.
Idara yetu hubadilisha pazia za milango katika kila tukio sambamba na kusafisha mapambo, ukuta, Kashi-Karbalai na sehemu zingine.