Idara ya Fatuma binti Aasadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea na ratiba ya kila wiki ya (Waulizeni wanaojua) baada ya kusimama ratiba hiyo wakati wa ziara ya Arubaini.
Inahudumia mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) kwa lengo la kuboresha usomaji wa Qur’ani tukufu.
Ratiba inavipengele vingi, kunakipengele cha masomo ya Fiqhi, maelekezo ya kidini kwa wanawake, usomaji wa kitabu katika idara ya maktaba ya Ummul-Banina (a.s), uwanja wa watoto (kufundisha watoto usomaji wa surat Fat-hah na sura fupi-fupi), na ugawaji wa machapisho mbalimbali kwa lengo la kuimarisha uwelewa wao.
Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) imegawa zawadi kwa washindi wa shindano la maana za maneno linalofanywa na idara kupitia usomaji wa Qur’ani wa kila siku kwenye mitandao ya kijamii.