Kituo cha utamaduni wa familia kinafanya warsha yenye anuani isemayo (Kurudi shuleni).

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kinafanya warsha yenye anuani isemayo (Kurudi shuleni).

Mkuu wa kituo Bibi Sara Hafaar amesema “Kituo kinafanya warsha yenye anuani isemayo (Kurudi shuleni) chini ya ukufunzi wa mtaalam ya saikolojia Dokta Maryam Abdulhussein, amefundisha mambo mbalimbali, umuhimu wa elimu ya msingi katika kujenga muelekeo wa mtoto, athari yake, jinsi ya kupambana na changamoto za kimakuzi na kisaikolojia katika umri huo”.

Akaongeza kuwa “Warsha imehusisha ugawaji wa vipeperushi maalum kwa wazazi vinavyo onyesha namna ya kuandaa chakula cha mtoto wakati wa asubuhi katika siku za masomo, ili kuweka uhusiano wa masomo na maisha ya kila siku”.

Warsha hiyo ni sehemu ya harakati za kituo katika uandaaji wa familia na kusaidia kambeni ya peleka watoto shule kwa mafanikio.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: