Idara ya Fatuma binti Asadi ya masomo ya Qur’ani inapokea wanafunzi wa mwaka mpya wa masomo.

Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inapokea wanafunzi wa mwaka mpya wa masomo 1446h.

Kiongozi wa idara hiyo Bibi Fatuma Mussawi wakati wa kupokea wanafunzi amesema, Kuna umuhimu mkubwa wa kutafuta elimu na kufuata mafundisho ya Ahlulbait (a.s), jambo hilo linahitaji utashi wa kweli.

Akabainisha kuwa idara inaratiba maalum na walimu wabobezi katika ufundishaji wa maarifa ya Qur’ani, Fiqhi, Aqida, Nahau, Akhlaq na masomo mengine ya kumjenga mwanamke kimalezi na kidini.

Idara inafanya kila iwezalo katika kuandaa kizazi chema cha wanawake wanaofuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s) na mafundisho ya Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: