Ombolezaji umeratibiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Ataba tukufu, unahusisha ufanyaji wa majlisi za kuomboleza asubuhi na jioni.
Mhadhiri wa majlisi Shekhe Ahmadi Abadi amesema “Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) ya wanawake ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Majlisi itadumu kwa muda wa siku tatu, inafanywa asubuhi na jioni, inaangazia historia ya Imamu Askariy (a.s) na kazi kubwa aliyofanya katika umma wa kiislamu pamoja na kueleza dhulma alizofanyiwa na watawala wa zama zake”.
Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya majlisi za kuomboleza katika kila tukio la msiba kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), kwa kueleza utukufu na historia zao takatifu.