Idara ya Dini inafanya ratiba ya kitamaduni kwa wageni wakike kutoka mkoani Basra.

Idara ya Dini katika Atabatu Abbasiyya, imefanya ratiba ya kitamaduni kwa wageni wakike kutoka mkoani Basra.

Kiongozi wa idara ya habari Bibi Rajaa Ali amesema “Idara imefanya ratiba ya kitamaduni kwa wanafunzi wa Daru-Taqwa Alqur’aniyya, mubalighat wake na taasisi ya Wai-Thaqafiyya kutoka mkoani Basra”.

Akaongeza kuwa “Ratiba inahusisha mashindano ya kifiqhi na kiaqida, yanayolenga kuimarisha uwelewa wa Ahlulbait (a.s) kwa washiriki sambamba na kugawa zawadi za kutabaruku kwao”.

Mwisho wa ratiba hiyo, wageni wamepongeza kazi nzuri ya kielimu inayofanywa na idara ya Dini ya kufundisha maadili mema kwa jamii ya wanawake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: