Kongamano litadumu kwa muda wa siku tatu, siku ya kwanza limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Liithi Ubaidi, ikafuatiwa na surat Fat-hah kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Lahnul-Iba, halafu ukafuata ujumbe wa rais wa chuo Dokta Judat Nuri Aljash’ami.
Mada za siku ya kwanza zimejikita katika kueleza “Usomaji na ufundishaji katika chuo.. uimara, udhaufu na changamoto zake”, vikao viwili vimeeleza viwango vya kimataifa vilivyofikiwa na chuo, idadi ya tafiti zilizoshiriki kwenye viwango vya kimataifa, maoni na michango ya kielimu kutoka kwa rais wa chuo na wakuu wa vitengo.
Kikao cha tatu kitachambua maoni na mapendekezo yaliyotolewa na wajumbe wa vyama vya walimu.