Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea na majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s).
Majlisi itafaywa kwa muda wa siku tatu chini ya usimamizi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Majlisi zinafanywa ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), chini ya uhadhiri wa Sayyid Ammaari Mussawi, ameongea kwa ufupi kuhusu historia tukufu ya Imamu (a.s) na msimamo wake katika kupambana na changamoto za jamii.
Majlisi imehitimishwa kwa kusoma tenzi na kaswida zinazoelezea msiba huo na kuamsha hisia za majonzi na huzuni kwa wapenzi wa Ahlulbait (a.s), zilizosomwa na Ali Saidi Mula katika mazingira yaliyojaa huzuni kwa wahudhuriaji.