Madrasat Fatuma binti Asadi (a.s) katika Atabatu Abbasiyya imeanza kusajili washiriki wa semina ya (Kwenda kwa Allah).
Jumamosi ya tarehe 14/9/2024m, itaanza semina hiyo itakayo kuwa inafanywa siku moja kwa wiki, watafundishwa Fiqhi, Aqida, Qur’ani na Akhlaq.
Kwa kila anaetaka kushiriki ajisajili katika madrasa iliyopo mtaa wa Mulhaq mkabala na mtaa wa Usrah, kituo cha Swidiqatu-Twahirah ghorofa ya nne, jirani na msikiti wa Swahibu Zamaan (a.f).
Madrasa imeandaa usafiri na mazingira ya kulea watoto wa washiriki bure.