Maukibu ya watu wa Karbala, imeomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) mbele ya malalo yake takatifu katika mji wa Samaraa.
Sayyid Badri Mamitha kutoka idara ya Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya amesema: “Maukibu ya watu wa Karbala kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya, imeomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) mbele ya malalo yake takatifu katika mji wa Samaraa”.
Akaongeza kuwa “Watu wa Karbala wamezowea kuomboleza kupitia maukibu ya pamoja, huja kumpa pole Imamu Mahadi (a.f) kutokana na msiba huo”. Akafafanua kuwa “Waimbolezaji wameimba qaswida na tenzi za kuomboleza zilizoamsha hisia za huzuni na majonzi”.
Akafafanua kuwa “Maukibu ya kuomboleza umejumuisha vikundi tofauti vya Husseiniyya kutoka Karbala pamoja na wakazi wa mkoa huo, baada ya matembezi wamefanya majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa harama ya maimamu wawili Askariyaini (a.s), imepambwa kwa tenzi na qaswida zilizoelezea msiba huo”.
Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kila iwezalo kuhudumia mazuwaru katika mji wa Samaraa chini ya utaratibu maalum na kwa ushiriki wa vitengo tofauti.