Kitengo cha matibabu kimehudumia zaidi ya mazuwaru 3000 katika mji wa Samaraa.

Kitengo cha matibabu katika Atabatu Abbasiyya kimehudumia zaidi ya mazuwaru 3000 katika mji wa Samaraa, wakati wa kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s).

Rais wa kitengo Dokta Haifaa Tamimi amesema: “Kitengo kinaendelea kutoa huduma za matibabu kwa mazuwaru wanaokuja katika mji wa Samaraa kuomboleza msiba wa Imamu Hassan Askariy (a.s) tangu siku tatu zilizopita, tumesha hudumia watu 3000 hadi sasa”.

Akaongeza kuwa “Kitengo kimeandaa vituo viwili vya kutolea huduma za afya, kituo kimoja cha wanaume na kingine cha wanawake”, akasema: “Huduma zinazotolewa zinahusisha huduma za dharura, kupima sukari, damu na kutoa dawa kulingana na hali ya mgonjwa”.

Akafafanua kuwa “Jopo la madaktari linaudwa na madaktari wa kike 14 na wanaume 35, wamekuja kutoka kwenye vituo vya afya vya mikoa tofauti, Diwaniyya, Hilla, Naswiriyya, Karbala. Wametoa huduma za matibabu, kinga pamoja na maelekezo ya afya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: