Mazuwaru wanaomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) katika mji wa Samaraa.

Mji wa Samaraa umeshuhudia makundi makubwa ya mazuwaru, kutoka ndani na nje ya Iraq, waliokuja kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) mbele ya malalo yake takatifu.

Mazuwaru wamefanya ziara na maombolezo, wameshindikiza jeneza la igizo kwa ushiriki mkubwa wa wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Katika maandalizi ya kupokea mazuwaru hao, mji umeimarisha ulinzi na utoaji wa huduma mbalimbali, hali kadhalika Maukibu zimesaidia kugawa chakula na vinywaji sambamba na kuandaa sehemu za kupumzika mazuwaru.

Atabatu Abbasiyya tukufu imekuwa ikitoa huduma mbalimbali katika mji wa Samaraa kwa siku nne mfululizo kwa kushirikiana na Atabatu Askariyya, kwa lengo la kurahisisha utekelezaji wa ziara na maombolezo kwa mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: