Maukibu ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, imeomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) katika mji wa Samaraa.
Mmoja wa wahudumu wa Maukibu Sayyid Hussein Swafi amesema “Maukibu ya Ataba mbili huomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) kwa kufanya matembezi katika mji wa Samaraa mbele ya malalo takatifu na hufatiwa na majlisi ya kuomboleza”.
Akaongeza kuwa “Maukibu hiyo hutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru watukufu, kama vile chakula na maji ya kunywa”.
Akafafanua kuwa “Maukibu haishii kugawa chakula na maji kwa mazuwaru peke yake, bali huandaa sehemu za kuswalia, hufanya majlisi za kuomboleza na hutoa maelekezo kwa vijana”.
Akasema kuwa, “Mahudhurio ya vijana mwaka huu yalikuwa makubwa”.










