Rais wa Iran ametembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais ya Iran Muheshimiwa Masudi Bazashkiyani ametembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pembezoni mwa ziara yake rasmi ya Iraq.

Muheshimiwa Bazashkiyani amepokewa na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Abbasi Mussawi, mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami na baadhi ya viongozi.

Kikao chao kimepambwa na video inayo onyesha miradi ya Atabatu Abbasiyya na huduma zinazotolewa kwa mazuwaru wa ndani na nje ya Iraq.

Wakazi wa ziara yake Muheshimiwa Bazashkiyani amesifu kazi kubwa inayofanywa na Atabatu Abbasiyya katika kuhudumia mazuwaru wa nchi tofauti, akasisitiza kuwa jambo hilo linaimarisha mafungamano ya kidini baina ya mataifa.

Atabatu Abbasiyya tukufu hupokea viongozi na wakuu wa nchi mbalimbali duniani katika kipindi chote cha mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: