Kwa kufanya kikao cha usomaji wa Qur’ani.. Majmaa-Ilmi imeomboleza kifo cha Imamu Askariy (a.s) katika wilaya ya Hindiyya.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeomboleza kifo cha Imamu Hassan Askary (a.s) kwa kufanya kikao cha usomaji wa Qur’ani.

Kikao hicho kimesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Hindiyya chini ya Majmaa-Ilmi.

Kikao cha usomaji wa Qur’ani kimefanywa katika Husseiniyya ya Haji Daudi Aali Salmaan, kimehudhuriwa na kundi kubwa la waumini, kimefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na Sayyid Abdullahi Husseini, kikafuata kisomo cha Yusufu Fatalawi na kuhitimishwa na msomaji wa Ataba mbili Haji Usama Karbalai.

Kumbuka kuwa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu hufanya vikao kama hivi katika kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) na matukio ya kidini, kwa lengo la kuimarisha mafungamano ya vizito viwili na kuvitumikia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: