Ugeni wa wanafunzi wa Dini umepongeza mafanikio ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Pongezi hizo zimetolewa baada ya kutembelea kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo, ambapo wameona mafanikio ya kitengo katika uhakiki na uandishi.
Ugeni umepokelewa na mkuu wa kituo Shekhe Swadiqu Khawilidi, ameeleza namna wanavyofanya uhakiki wa nakala-kale na kazi kubwa wanayofanya ya kuhuisha turathi za kiislamu katika mji wa Hilla.
Wanafunzi wamepongeza machapisho ya Markazi na nafasi yake katika kutunza historia ya mji na wanachuoni wake kwa njia za kisasa.
Kituo cha turathi hupokea wageni mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano na pande zote katika sekta ya utamaduni, elimu na turathi.