Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imeanza kupokea wanafunzi wa mwaka mpya wa masomo.
Idara imepokea wanafunzi katika ofisi zake zilizopo kwenye kituo cha Swidiqatu Twahirah (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Idara hufundisha masomo tofauti kama vile, mbinu za kutoa muhadhara, mahadhi ya Husseiniyya, elimu ya Fiqhi, hukumu za usomaji wa Qur’ani tukufu, elimu ya Aqida na Akhlaq.
Ratiba maalum inayo onyesha masomo yatakayo fundishwa imeandaliwa.
Idara imesema kuwa usajili unaendelea katika madarasa ya Maahadi ya wahadhiri wa Husseiniyya, kwa lemgo la kupokea wanafunzi wapya na kuwaendeleza katika masomo tofauti.