Atabatu Abbasiyya imefanya kikao cha kutambulisha uboreshaji wa maendeleo ya kiidara.

Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kikao cha kutambulisha uboreshaji wa maendeleo ya kiidara unaofanywa.

Kazi hiyo inasimamiwa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Ataba tukufu.

Rais wa kitengo Dokta Muhammad Hassan Jaabir amesema “Atabatu Abbasiyya imefanya kikao cha kutambulisha mradi wa uboreshaji na utaratibu wa ndani, sambamba na kufafanua mafanikio yanayopatikana kwa washiriki wake”.

Akaongeza kuwa “Mkutano unaongozwa na wajumbe wa kamati kuu, Sayyid Jawadi Hasanawi na Dokta Abbasi Didah Mussawi, aidha wamehudhuria marais wa vitengo na wasaidizi wao kwa ajili ya kujibu na kutoa maelezo kuhusu vitengo vyao”.

Akafafanua kuwa “Mkutano umejikita katika kufafanua utendaji kaji na kukamilisha mitihani ya wanafunzi wapya”, akasema “Kuna muda wa mwezi mmoja wa majaribio kwa ajili ya kuangalia uwezo wa wanafunzi wapya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: