Atabatu Abbasiyya imeweka mazingira ya furaha katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume na Imamu Swadiq (a.s).

Watumishi wa kitengo cha majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, wameweka muonekano unaoashiria furaha ya kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s).

Kiongozi wa idara ya haram chini ya ofisi ya umeme Sayyid Haidari Jawadi amesema “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Ataba tukufu, tumeweka mazingira ya furaha katika kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swaqiq (a.s), tumefunga taa za rangi zenye ukubwa tofauti ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwenye njia zinazoelekea haram kwa namna ambayo zinaakisi furaha kwa tukio hili adhim”.

Akaongeza kuwa “Taa za rangi zilizofungwa ndani ya haram tukufu na kwenye barabara zinazo elekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zipo zaidi ya elfu 11”.

Atabatu Abbasiyya inaandaa hafla kubwa ya kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s) katika uwanja wa mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mwezi 16 Rabiul-Awwal 1446h sawa na 20/9/2024m.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: