Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya semina ya kuwajengea uwezo walimu wake kuhusu mtazamo mpya wa malezi.
Kiongozi wa Maahadi Bibi Manaar Aljaburi amesema “Maahadi imefanya semina ya kuwajengea uwezo zaidi ya walimu wake (100), kuhusu mtazamo mpya wa malezi”.
Akaongeza kuwa “Semina itadumu kwa muda wa siku sita, kila siku kutakuwa na mihadhara mitatu kutoka kwa walimu waliobobea katika elimu ya saikolojia, wanaelekeza malezi bora na mbinu za kunufaika na makuzi ya wanafunzi katika hatua zote za ukuaji wao”.