Chuo kikuu cha Al-Ameed kimeanza kupokea wanafunzi wa mwaka mpya wa masomo (2024 – 2025) katika mazingira mazuri ya mwaka wa masomo yanayoendana na mtazamo wa chuo katika kuhudumia jamii.
Chuo kilikuwa kimeshatangaza utayali wake wa kupokea wanafunzi wa mwaka mpya wa masomo baada ya kukamilisha maandalizi yote muhimu.
Chuo kimeandaa kumbi za madarasa na maabara kwa kuweka vifaa vya kisasa vinavyo saidia kuongeza ubora katika ufundishaji na usomaji wa wanafunzi.
Mwaka mpya wa masomo katika chuo kikuu cha Al-Ameed, umepambwa na maktaba maalum ya wanafunzi wa bweni yenye miongozo ya masomo yote.
Chuo kinafanya kila kiwezalo katika kuinua kiwango cha elimu za wanafunzi wake.