Sayyid Swafi ametoa wito wa kuongeza juhudi katika kuhuisha turathi za wanachuoni wa Imamiyya kwenye elimu tofauti.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, ametoa wito wa kuongeza juhudi katika kuhuisha turathi za wahenga wa Imamiyya kwenye elimu tofauti, hususan kwenye sekta ya Aqida na kutetea Uimamu.

Ameyasema hayo alipokutana na wageni kutoka taasisi ya Uimamu ya kimataifa kutoka Iran, ambao ni Shekhe Najmu-Dini Twabsi, Shekhe Dokta Muhammad Taqi Subhani mkuu wa taasisi, kundi la wahakiki na watumishi wa taasisi, wameongea mambo tofauti kuhusu turathi za wanachuoni wakubwa na umuhimu wa kuzifundisha katika vizazi vijavyo.

Muheshimiwa Sayyid Swafi ameanza kwa kukaribisha wageni, akasisitiza umuhimu wa kuhuisha turathi za wahenga wa Imamiyya kwenye elimu tofauti, hususan elimu ya Aqida na kutetea Uimamu, kutokana na umuhimu wa kumuelezea kiongozi wa waumini (a.s).

Akabainisha kuwa, wanachuoni hao walifanya kazi kubwa na kujitolea maisha yao katika kuwatetea Maimamu wa Ahlulbait (a.s), kuhuisha turathi zao na kuwakumbuka ni wajibu kwetu, hususan turathi zinazohusu Aqida, nyingi bado hazijafikiwa, kama vile muheshimiwa Miri Haamid Husseini mwenye Abaqaati na Sayyid Abdul-Hussein Sharafu-Dini, wasingeweza kubobea kwenye Aqida kama wasingekuwa wabobezi wa Fiqhi iliyo wawezesha kutoa hukumu za kisheria, hivyo wakasimama imara katika kutetea Uimamu wa kiongozi wa waumini na Maimamu wengine (a.s), pamoja na mambo mengi yaliyozushwa kwenye sekta hiyo.

Akapongeza kazi kubwa inayofanywa na taasisi ya Uimamu katika kuhuisha turathi za wanachuoni, akasisitiza utayali wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kusaidia sekta hiyo.

Naye Shekhe Twabsi akaongea kuhusu umuhimu wa kuhuisha turathi za wanachuoni katika sekta ya Aqida, ili kizazi kipya kifahamu kazi kubwa iliyofanywa ya kulinda Aqida, aidha amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria ya kuhuisha turathi za wanachuoni, kupitia miradi ya kuhakiki nakala-kale na kufanya makongamano na nadwa za kielimu.

Shekhe Subhani pia akapongeza kazi zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya ya kuhuisha turathi za wanachuoni wote kwa ujumla, na kufanya makongamano na nadwa, ikiwemo nadwa ya mwenye Abaqaati inayotarajiwa kufanywa kesho siku ya Alkhamisi katika jengo la Murtadha mjini Najafu sambamba na kazi ya kukusanya nakala-kale kutoka nchi tofauti duniani kwa ajili ya kutumiwa na watafiti.

Mwisho wa kikao hicho Shekhe Subhani akakabidhi turathi za Miri Haamid Hussein Abaqaati kwa Sayyid Swafi, naye akashukuru wageni hao kumtembelea na akawatakia mafanikio mema katika kazi yao ya kuhuisha turathi za wanachuoni watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: