Kitengo cha maarifa kimemaliza semina ya Aqida kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimemaliza semina ya Aqida kwa zaidi ya watumishi 200.

Kiongozi wa idara ya habari za maarifa Sayyid Basim Muhammad amesema “Semina imepambwa na maswali ya kidini na kiaqida, yaliyokuwa yanajibiwa na watumishi kisha majibu kupelekwa katika kamati maalum ya kusahihisha na kutoa alama (max)”.

Akaongeza kuwa “Semina imepata muitikio mkubwa na baadhi ya vitengo vimeonyesha nia ya kushiriki watumishi wao ili kuwaongezea maarifa ya Dini katika zama hizi zilizojaa changamoto nyingi za kijamii”.

Mmoja wa watumishi wa idara ya habari za maarifa Sayyid Karaar Yaasi Khadhwiri amesema “Semina inalenga kujenga uwelewa wa kidini na kitamaduni kwa watumishi, imepambwa na mihadhara ya kidini kutoka kwa Shekhe Muhammad Jafari Twabasi na imedumu kwa siku saba”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: