Kitengo cha mahusiano kimeandaa ratiba ya wanafunzi kutoka Misaan

Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa ratiba ya wanafunzi kutoka mkoa wa Misaan.

Mmoja wa watumishi wa kitengo Sayyid Amiri Haadi Jaliil amesema “Idara ya mahusiano imeandaa ratiba ya wanafunzi wa sekula kutoka Misaan”, akasema “Hiyo ni sehemu ya kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu na shule za Iraq”.

Akaongeza kuwa “Ratiba imepambwa na vipengele vingi, ikiwepo utowaji wa mihadhara ya kidini na kitamaduni, kutembelea miradi ya Ataba tukufu, shirika la teknolojia ya viwanda na kilimo cha kisasa Khairul-Juud, kiwanda cha madirisha ya makaburi ya Ataba tukufu”.

Kiongozi mkuu wa ratiba hiyo Sayyid Haidari Hassan amesema, “Tumetembelea baadhi ya miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu”, akaongeza kuwa “Miradi hiyo inaendana na maendeleo ya dunia kwenye sekta tofauti”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: