Kiongozi wa idara ya kuhifadhi katika Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa Shekhe Ali Rawii amesema “Majmaa-Ilmi imefanya shindano la nne likiwa na washiriki 50 wanaohifadhi Qur’ani tukufu”.
Akaongeza kuwa “Washuriki wamegawika katika makundi matano, ambayo ni: kundi la waliohifadhi juzuu 5, juzuu 10, juzuu 15, juzuu 20 na juzuu 30”.
Shindano linalenga kuimarisha uwezo wa kuhifadhi Qur’ani tukufu kwa wanafunzi, na kuangalia uwezo wao wa hifdhu, sambamba na kuwashajihisha kushiriki kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa.