Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kimefanya muhadhara kuhusu mitandao ya kijamii na athari yake kwa wanafunzi, mbele ya ugeni wa wanafunzi kutoka mkoa wa Misaan.
Mhadhiri Sayyid Jasaam Saidi amesema “Muhadhara umejikita katika kueleza athari za mitandao ya mawasiliano ya kijamii kwa wanafunzi na namna ya kulinda kumbukumbu na kujiepusha na usahaulifu”.
Akaongeza kuwa “Muhathara umeeleza hatari za video fupi, visa vifupi, youtube na kutahadharisha kuziangalia, sambamba na kueleza namna ya kunufaika na mitandao kimasomo kwa wanafunzi”.
Kiongozi mkuu wa sekta ya sekula Sayyid Haidari Shekhe Hassan amesema “Muhadhara ulikuwa na faida kubwa, kwani umejikita katika kueleza umuhimu wa kutunza akili na kujiepusha na mitandao ya kijamii yenye maudhui mbaya na namna ya kunufaika nayo kimasomo”.