Makamo rais wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu Dokta Ibrahim Tamimi amesema “Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa-Ilmi, imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika kuadhimisha mazazi ya Mtume (s.a.w.w)”.
Akaongeza kuwa “Hafla imeshuhudia ugawaji wa zawadi kwa baadhi ya vitengo vya Ataba tukufu, vilivyo shiriki katika kufanikisha semina za Qur’ani katika majira ya joto”.
Hafla imepambwa na usomaji wa tenzi na mashairi.
Imelenga kuonyesha vipaji vya wasomaji wa Qur’ani na kushajihisha utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii.