Kitengo cha kusimamia Haram kimegawa mauwa kwa mazuwaru katika kuadhimisha mazazi ya wakweli wawili (a.s).

Kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimegawa pipi na mauwa kwa mazuwaru katika kuadhimisha mazazi ya Mtume (s.a.w.w) na Imamu Swadiq (a.s).

Katika kila tukio la kuadhimisha kuzaliwa kwa mtukufu katika nyumba ya Mtume (s.a.w.w), kitengo hugawa pipi na mauwa kwa mazuwaru wanaokuja kutoa pongezi na kumzuru (Qamarul-Ashirah) Mwezi wa familia (a.s).

Atabatu Abbasiyya imefanya hafla kubwa ya kuadhimisha mazazi ya Mume Muhammad na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s) katika uwanja wa mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na viongozi wa Atabatu Abbasiyya, marais wa vitengo vyake, ugeni kutoka Atabatu Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya na kundi kubwa la watumishi wa malalo na mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: