Msaidizi wa kiongozi mkuu wa eneo hilo, Mhandisi Dhiyabu Sharifi amesema: “Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya Mtume (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s) katika eneo la vitalu vya Alkafeel”.
Akaongeza kuwa “Hafla umehusisha vipengele mbalimbali, ikiwemo mashairi na tenzi, mbele ya kundi kubwa la wakazi wa Karbala, sambamba na ugawaji wa zawadi na mauwa kwa wahudhuriaji”.
Akasema: “Atabatu Abbasiyya hufanya maadhimisho ya matukio mbalimbali yanayohusu watu wa nyumba ya Mtume na Maimamu watakasifu (a.s)”.