Ufunguzi wa tawi la Qabsu katika mkoa wa Korbala, umehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, baadhi ya viongozi wa Dini na Hauza.
Kiongozi mkuu wa taasisi hiyo Shekhe Twariq Baghdadi amesema “Taasisi ya Qabsu imefungua tawi katika mkoa wa Karbala, sambamba na maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Tawi linamajukumu mengi, ukizingatia mji mtukufu wa Karbala hupokea mamilioni ya mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kila mwaka, litaendesha program mbalimbali kwa lengo la kujenga uwelewa wa kidini na kushikamana na Ahlulbait (a.s)”.
Akaendelea kusema “Hilo ni eneo la msingi katika utendaji wa taasisi, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kulinda tunu za uislamu katika mazingira ya vita vya kitamaduni na kifikra”