Mkuu wa Maahadi ya Kingston ya Uingereza amepongeza utunzaji wa mali-kale katika makumbusho ya Alkafeel

Mkuu wa Maahadi ya Kingston ya Uingereza katika mji wa Dubai Dokta Naadir Alhamdu, amepongeza utunzaji wa mali-kale katika makumbusho ya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Ametoa pongezi hizo katika ziara aliyofanya, akiongozwa na rais wa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya Dokta Muhammad Hassan Jaabir, mbele ya rais wa Makumbusho Sayyid Swadiq Laazim Zaidi.

Muheshimiwa Naadir, amepongeza teknolojia inayotumika katika kutunza mali-kale za makumbusho pamoja na namna zilivyopangwa ndani ya makumbusho.

Makumbusho hupokea idadi kubwa ya wageni kutoka ndani na nje ya Iraq, watumishi wa Makumbusho huelezea historia ya makumbusho na mali-kale zilizomo katika zama tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: