Ofisi ya Muheshimiwa Marjaa-Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, imetoa tamko kuhusu mashambulizi ya Iszael nchini Lebanon.
Ifuatayo ni nakala ya tamko hilo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.
Katika siku hizi ngumu kwa raia wa Lebanon, ambapo wanaendelea kushambuliwa na Izrael kwa namna mbalimbali, hivi karibuni vifaa vya mawasiliano binafsi vimeripuka na kuua watu wengi sambamba na kushambulia nyumba za makazi ya watu na kuuwa watoto na wanawake, mashambulizi makubwa yamefanywa katika vitongoji mbalimbali na kuuwa idadi kubwa ya watu na wengine wengi kujeruhiwa, huku watu wengi wakilazimika kukimbia makazi yao. Marjaa-Dini mkuu anaungana na raia wa Lebanon na kuwapa pole, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awahami na kuwalinda kutokana na njama za maadui, awarehemu mashahidi na kuwaponya haraka majeruhi.
Tunaomba kusimamishwa kwa mashambulizi hayo na kulinda raia wa Lebanon na maafa, tunatoa wito kwa waumini watoe misaada ya kibinaadamu kwa raia wa Lebanon.
Mwenyezi Mungu ailinde Lebanon na raia wake kwa kila baya.
19 Rabiul-Awwal 1446h sawa na 23 Septemba 2024m.
Ofisi ya Sayyid Sistani – Najafu-Ashrafu.